Kuhusu sisi
Fareedahmoh ni chapa ya kizawa ambayo tuliangalia kuhusu kuboresha afya na kuongeza nguvu kazi ya taifa yapo maeneo mengi yenye kuhitaji nguvu nasi tukachagua eneo la afya kupitia chakula cha mlaji wa kila siku. Nia ni kumpa mlaji afya na sio utamu pekee kupitia bidhaa husika.
Hivi sasa tunayo bucha inayohudumia watu kwa bidhaa na mahitaji ya jikoni, kuhakikisha kuwa mlaji anapata kilicho bora kwa afya yake lakini kilicho halisi ili kupata ladha na virutubisho vyake pia. Afya yako ni muhimu sana na chakula tunachokula ni dawa ndani ya maiili yetu hivyo tunahitaji sasa kuingiza mwilini kile kilichobora kuanzia upatiakanaji uandaaji lakini hadi ulaji wenyewe. Kwetu Fareedahmoh tunaamini Afya kwanza halafu utamu baadae.